Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke anayekumbatia watoto njiti azidi kuwagusa Watanzania

SD MAMA WATOTO NJITI Mwanamke anayekumbatia watoto njiti azidi kuwagusa Watanzania

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis amemtembelea Mwanadada Mariam Mwakabungu (25) anayejitolea kukumbatia watoto Njiti waliotelekezwa na mama zao katika Hospitali ya Amana, Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis amemtembelea Mariam na kumpatia kiasi cha Sh. Milioni 1 na kumtia moyo kwa kazi anayoifanya hospitalini hapo.

Mariam ametembelewa hospitalini hapo ikiwa ni siku chache tangu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumpongeza na kupatia kiasi cha Sh. Milioni 2.

Akizungumza mara baada ya kumtembelea kwenye wodi ya watoto hao katika hospitali hiyo, Mhe. Mwanaidi amesema kuwa lengo la kufika katika Hospitali hiyo ni kumpongeza pamoja na kumtia moyo ili kuhakikisha anakuwa na amani katika malezi ya watoto hao.

"Tumekuja katika Hospitali hii ya Amana kumsaidia huyu mama pamoja na kumpongeza na sisi kama wizara tunaungana na Rais Samia kuhakikisha mama huyu anaishi vizuriā€ alisema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live