Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke aishtaki serikali miaka 42 baada ya kumfunga kizazi….Ilikuwaje?

2357 Mesothelioma Law Firm 660x400

Thu, 1 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Katika hali ya kushangaza mwanamke mmoja raia wa Japan ameishtaki serikali ya nchi hiyo kwa kumfunga kizazi mwaka 1972 kipindi ambacho alikuwa na umri wa miaka 15.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo alifungwa kizazi ni mmoja kati ya wanawake wengine 250 waliofungwa kizazi kipindi hicho chini ya sheria ambayo haitekelezwi kwa sasa.

Kwenye miaka hiyo ya 1970 inaelezwa kuwa wanawake waliokuwa na matatizo ya vichaa au ukoma na yeye alipatikana na tatizo la kasoro katika ubongo ambalo lilikuwa la kurithi.

Taarifa za matukio hayo pia zinaonesha kuwa takribani 16,500 kati ya wanawake hao walidaiwa kufanyiwa upasuaji huo bila idhini yao huku baadhi yao walikuwa wadogo hadi umri wa miaka tisa.

“Maswali mengi ya Wabunge nayoulizwa yanahusu ujenzi wa Mahakama” Prof. Kabudi



Chanzo: millardayo.com