Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa udaktari apandikiza Bluetooth sikioni kuiba mtihani

Huyu Balaa.jpeg Mwanafunzi apandikiza Bluetooth sikioni kuiba mtihani

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku za mwizi ni arobaini, Waswahili husema! Mwanafunzi mmoja zilifika baada ya kupatikana amepandikiza kifaa cha Bluetooth kwenye sikio lake ili kufanya udanganyifu katika mtihani.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa mwisho wa masomo ya udaktari, alikuwa akifanya mtihani huo katika Chuo cha Mahatma Gandhi Memorial alifumaniwa wakati msimamizi wa nje wa mtihani huo na kikosi chake walipofika katika shule hiyo kwa kushtukiza.

Spika ya simu ilipatikana ikiwa imepandikizwa kwenye sikio lake kwa njia ya upasuaji wakati wakati wa mtihani huo wa General Medicine siku ya Jumatatu, Februari 21, 2022.

Mkuu katika Chuo hicho, Sanjay Dixit amesema kwamba mtihani huo ulikuwa jaribio la mwisho kwa mwanafunzi huyo baada ya kurudia mara kadhaa tangu ajiunge na chuo hicho miaka 11 iliyopita.

Gazeti la The Independent liliripoti kuwa wakuu wa chuo hicho walishindwa kupata kifaa cha Bluetooth walipokuwa wakimkagua mwanafunzi huyo ambaye jina lake lilihifadhiwa, lakini uchunguzi unaendelea na ukikamilika atafikishwa katika vyombo vya sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live