Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaleta adha ya usafiri Mbagala

56592 Pic+mvua

Fri, 10 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kuanzia leo alfajiri Ijumaa Mei 10, 2019 imesababisha adha ya usafiri kwa wakazi wa Mbagala kutokana na daladala nyingi kutofanya kazi.

Mwananchi limeshuhudia makundi ya watu yakiwa vituoni wakisubiri usafiri bila mafanikio.

Wakati wakionekana kuwa na nyuso za kukata tamaa huku wakiloana, daladala zimeonekana zikiwa zimeegeshwa maeneo mbalimbali.

Changamoto inaonekana kubwa zaidi kwa wanafunzi huku baadhi yao wakionekana kusindikizwa shuleni.

Sehemu kubwa ya barabara ya Kilwa hasa eneo la Mbagala Zakhiem na Mbagala Rangi tatu zimefurika maji hali inayosababisha magari kupita kwa tabu.



Chanzo: mwananchi.co.tz