Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuguzi asimamishwa kwa kukiuka maadili

3a59e4988bfc31e32922a505e9a4d726.jpeg Muuguzi asimamishwa kwa kukiuka maadili

Mon, 11 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga imemsimamisha kazi muuguzi, Michelina Mduda kwa kukiuka maadili na miongozo ya taaluma.

Taarifa ya halmashauri hiyo ilieleza kuwa Julai 3 mwaka huu muuguzi huyo alimsababishia madhara mjamzito aliyefika kujifungua katika zahanati ya Mtimbwa kwenye kata ya Matanga. Ilieleza kuwa imesikitishwa na ukiukwaji maadili na miongozo ya kitaaluma uliofanywa na Michelina.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Samson Medda kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika halmashauri hiyo ilieleza kuwa Michelina amesimamishwa kuanzia Julai 6 mwaka huu wakati shauri lake likishughulikiwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania. “Ofisi imempatia Michelina Mduda notisi ya kusimamishwa kutoa huduma za uuguzi na ukunga iliyotolewa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania,” ilieleza taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live