Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mungu mkubwa! Pacha walioungana kifuani watenganishwa Muhimbili

Images (7).jpeg Mungu mkubwa! Pacha walioungana kifuani watenganishwa Muhimbili

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: Mwananchi

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikisha upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha walioungana kifuani Rehema na Neema.

Upasuaji huo uliodumu kwa saa 7, ulioanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 9 alasiri, umefanikiwa licha ya ugumu na changamoto kubwa kwa watoto hao kuungana ini, moyo na baadhi ya tishu za ndani.

Upasuaji huo uliofanyika kwa mafanikio umefanyika leo Ijumaa Julai Mosi 2022 kwa ushirikiano kati ya wataalamu wa afya 31 kutoka Tanzania na Ireland ambao wanatokea Shirika la Operation Child Life.

Akizungumza na vyombo vya habari, Daktari bingwa wa upasuaji watoto hospitalini hapo, Zaitun Bokhari amesema upasuaji huo umefanywa na madaktari bingwa wa upasuaji watoto wadogo 12.

“Madaktari wa usingizi sita, madaktari wa kutengeneza ngozi ‘plastic surgery’ wanne, madaktari ambao kazi yao kuangalia mfumo mzima wa watoto unakwenda vizuri wawili na wauguzi 6,” amesema.

Upasuaji wa kutenganisha pacha walioungana ulifanyika kwa mara ya kwanza nchini mwaka 1994 na wa pili ni mwaka 2018.

Chanzo: Mwananchi