Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili yatumia dawa za Sh72 bilioni tangu 2015

85036 Mimba+pic Muhimbili yatumia dawa za Sh72 bilioni tangu 2015

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetumia dawa za Sh72 bilioni tangu mwaka 2015.

Ongezeko hilo la kipindi cha miaka minne limetokana na bajeti kuongezwa kutoka Sh500  milioni hadi Sh700 milioni kwa mwezi hadi Sh1.5 bilioni tangu Rais John Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania Novemba 5, 2015.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya Magufuli.

Amesema huduma ya dawa ilikuwa changamoto kubwa lakini  baada ya maagizo kadhaa ya kiongozi huyo kuhusu kuboresha huduma hiyo, mambo yalikuwa mazuri.

“Hospitali imetekeleza agizo hili kwa kuboresha upatikanaji wa dawa na hadi sasa wagonjwa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa ya Hospitali ukilinganisha na wastani wa asilimia 40 kabla ya uboreshaji huo,” amesema.

Amesema hospitali ilianzisha mfuko maalumu kwa ajili ya dawa  na fedha zinazopatikana kutokana na mauzo ya dawa hutumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa.

">“Kwa sasa Sh1.5 bilioni hutumika kununua dawa kila mwezi sawa na Sh18 bilioni kwa mwaka. Katika kipindi cha miaka minne, Hospitali imenunua na kuwapa wagonjwa dawa za Sh72 bilioni, wagonjwa wanaokosa dawa katika maduka yetu, Hospitali inanunua haraka ili wapate dawa,” amesema Profesa Museru.

Chanzo: mwananchi.co.tz