Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili yapandikia figo kwa wagonjwa 93

Figo Nguruwe Muhimbili yapandikia figo kwa wagonjwa 93

Sat, 30 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagonjwa 93 wamepandikizwa figo nchini, tangu kuanza kwa huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Benjamini Mkapa.

Kati ya wagonjwa hao 67 wamepandikizwa Muhimbili, huku 26 katika hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.

Asilimia 10 ya watu duniani wanaishi na magonjwa sugu ya figo, huku asilimia 50 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 75 wana ugonjwa sugu wa figo.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifello Sichalwe, wakati wa ufunguzi wa kongamano la kisayansi la wauguzi wataalamu wa Afrika lililofanyika jijini Dar es Salaam.

"Dhima ya kongamano hili ni kuleta maendeleo ya huduma ya magonjwa ya figo duniani, ambapo jukumu la elimu na ubunifu kwenye nchi za Afrika na dhima hii imekuja kwa wakati muafaka, ambapo Tanzania inaenda kuimarisha na kupanua upatikanaji wa huduma za figo," amesema Dk. Sichalwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live