Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili yaanza upandikizaji uboho

Muhimbilipic Muhimbili yaanza upandikizaji uboho

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imeanza rasmi upasuaji wa upandikizaji wa uboho, hatua inayoleta matumaini mapya kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na saratani.

Pia, ikijulikana kama upandikizaji wa seli ya shina, upandikizaji wa uboho ni matibabu ambayo huchukua nafasi ya uboho wa mgonjwa na seli zenye afya.

Seli zinazobadilishwa zinaweza kutoka kwa mwili wa mgonjwa mwenyewe au kutoka kwa mtu mwingine.

Shughuli ya upandikizaji inaweza kutumika kutibu aina fulani za saratani kama vile leukemia, myeloma na lymphoma, seli mundu na magonjwa mengine ya damu na mfumo wa kinga ambayo huathiri uboho.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa huduma ya upandikizaji wa uboho nchini Tanzania jana, Mkuu wa kitengo cha Hematology na daktari bingwa wa magonjwa ya damu MNH, Dk Stella Rwezaura alisema hospitali hiyo hadi sasa imeshafanya upasuaji huo kwa wagonjwa watano, na kwamba kwa sasa wengine watano wanaendelea kusubiri katika orodha.

“Ulikuwa ni mchakato mrefu uliohusisha wataalam mbalimbali wa afya kutoka idara mbalimbali kuhakikisha upandikizaji wa uboho unafanikiwa na unatunzwa vyema. Tulifanya kazi kwa pamoja na tunafurahi kwa hatua tuliyopiga kama taifa,” alisema Dk Rwezaula.

Alisema mgonjwa huwekwa wazi kwa michakato na taratibu kadhaa kabla ya upandikizaji wa uboho kufanyika.

“Inaanza na utambuzi wa ugonjwa kisha ‘chemotherapy’ inatumika kwa muda wa kati ya miezi minne hadi sita. Tiba kama hiyo inapaswa kuzingatia dawa zote zinazoruhusu upandikizaji wa uboho kutokea,” alisema.

Alisema matibabu yanaendelea huku wagonjwa wakiendelea kupata nafuu hadi vipimo vya afya vitakapothibitisha kuwa mgonjwa amepona kabisa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof Lawrence Museru, kuanza kwa upandikizaji wa uboho nchini Tanzania kunamaanisha kuwa mgonjwa ataweza kuokoa karibu Sh180 milioni kama atakwenda kutibiwa nchini India.

Kwa Muhimbili alisema gharama ni Sh70 milioni

Mgonjwa angetumia Sh250 milioni kupata matibabu ya uboho nje ya nchi hususani India lakini MNH, mgonjwa mmoja analipa takriban Sh70 milioni.

Chanzo: mwananchidigital