Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili, yaanza mafunzo matumizi ya vifaa

Muhimbili Langooo.jpeg Muhimbili, yaanza mafunzo matumizi ya vifaa

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Julieth Magandi amefungua mafunzo ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya vifaa vya kufuatilia mwenendo wa upumuaji wa mgonjwa na namna ya kumhudumia mgonjwa kwa kutumia mashine hizo. - Mafunzo hayo yanatolewa na hospitali hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya utengenezaji na usambazaji vifaa tiba ya Mindray na Anudha ambapo yameshirikisha wataalamu kutoka wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, vyumba vya upasuaji, idara ya wagonjwa wa dharura, idara ya usingizi na ganzi pamoja na wataalamu wa vifaa tiba (biomedical engineers). - Dk Magandi amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii na kubadilishana uzoefu ili wakaendelee kuboresha huduma katika kuwahudumia wagonjwa katika maeneo yao ikiwa ni utekelezaji wa serikali wa kuendelea kutoa huduma bora za afya. - “Wito wangu kwenu, hakikisheni mnajifunza kwa juhudi zote ili mjue kutumia vifaa hivi vizuri iwasaidie kutibu wagonjwa kwa usahihi na pia mjue ni namna gani mnaweza kuvitunza vifaa hivi ili viweze kudumu kwa muda mrefu”,Amesisitiza Dk Magandi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live