Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili waendesha mafunzo ya siku mbili

Muhimbili Waendesha Mafunzo Ya Siku Mbili.jpeg Muhimbili waendesha mafunzo ya siku mbili

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Wataalamu cha Utoaji Tiba ya Magonjwa ya Dharura Tanzania (EMAT) kimeendesha mafunzo ya siku mbili kwa madereva wanaondesha magari ya dharura, wauguzi na wahudumu wa afya kwa lengo la kuboresha huduma za dharura hospitalini hapa.

Akifungua Mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa Idara ya Utawala Bi. Teckla Msina amesema mafunzo yatasaidia kuendelea kuboresha utendaji kazi miongoni mwa wadau waliopo katika mnyororo wa huduma za dharura.

“Tumeamua kuwashirikisha ninyi katika mafunzo haya kwa kutambua kuwa ni wadau muhimu katika kutoa huduma za dharura hivyo ni lazima tuhakikishe tunafuatilia kwa makini mafunzo haya na kuyafanya kwa vitendo yale yote yanayofundishwa ili kuendelea kuboresha huduma zetu zaidi,” ameongeza Bi. Teckla

Aidha, Bi. Tekla amewataka madereva wanaoendesha magari ya dharura kuzingati sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali za kwakuwa asilimia kubwa ya ajali hizo zinazotokea zinasababishwa na uzembe wa madereva ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani.

Mafunzo hayo yametolewa kwa nadharia na vitendo na yamehusisha watoa huduma 25 ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo usalama barabarani, utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na namna ya kumuhudumia mgonjwa ndani ya gari la wagonjwa wa dharura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live