Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili kupandikiza wagonjwa watano figo Oktoba

Upasuajiiii (600 X 398) Muhimbili kupandikiza wagonjwa watano figo Oktoba

Sat, 30 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inatarajia kufanya huduma ya kibingwa na bobezi ya upandikizaji figo kwa wagonjwa watano kuanzia Oktoba 2 hadi 6, 2023.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji, Dk Godlove Mfuko upandikizaji huo ni wa kisasa ambapo utahusisha kutoa figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia njia ya matundu, utaalamu ambao hapa nchini unafanyika MNH-Mloganzila pekee ukilinganisha na hospitali zingine ambazo humfanyia upasuaji mchangiaji.

Dk Mfuko ameongeza kuwa upandikizaji huu unaohusisha kutoa figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia matundu madogo unamsaidia mchangiaji kutokua na kovu kubwa, kupona mapema na kurudi katika majukumu yake mapema zaidi ukilinganisha na upandikizaji uliozoeleka ambao mchangiaji hufanyiwa upasuaji.

“Hii ni mara ya pili kwa hospitali yetu kupandikiza figo kwa njia ya matundu, hapo awali tuliwafanyia wagonjwa watatu ambao kwa sasa wanaendelea vizuri na mpango wetu ni kufanya upandikizaji wa aina hii kila mwezi,” amebainisha Dk Mfuko.

Dk Mfuko amebainisha kuwa upandikizaji huu umewezekana kutokana na serikali kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani, kununua vifaa tiba na kujenga miundombinu wezesheshi katika kutoa huduma za upandikizaji figo MNH Mloganzila, jambo ambalo limesaidia kupunguza gharama kwa wagonjwa kwa zaidi ya asilimia 50 endapo wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa upandikizaji.

Upandikizaji huo wa figo unafanywa na wataalamu wa ndani kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka nchini Korea Kusini Prof. Park Kwan Tae chini ya Taasisi ya KOFIH ya Korea Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live