Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto

26559 Pic+muhimbili TanzaniaWeb

Sun, 11 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 10 ambao wana matatizo ya kusikia kuanzia kesho Jumatatu, Novemba 12 hadi 16, 2018.

Idadi hiyo itafanya watoto 21 ambao wamefanyiwa upandikizaji huo tangu huduma hiyo ianze kutolewa Juni mwaka 2017.

Watoto hao watapandikizwa vifaa vya usikivu baada ya wataalam kuwafanyia uchunguzi wa kina pamoja na wazazi kupatiwa ushauri wa kitaalamu.

Daktari Bingwa wa upasuaji wa masikio, pua na koo wa hospitali hiyo, Dk Edwin Liyombo amesema maandalizi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto hao yamekamilika.

Dk Liyombo amesema leo Jumapili wamefanya kikao cha pamoja na wazazi wa watoto hao ili kuwaandaa na kuwapatia maelekezo jinsi ya kuwa karibu zaidi na watoto hao ili waweze kusikia vizuri na kuzungumza baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu.

“Wazazi wanatakiwa kuwafuatilia kwa karibu watoto baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu. Zinahitajika nguvu za ziada ili watoto waweze kuzungumza vizuri na kusikia,” amesema.

Kwa mujibu wa Dk Liyombo wastani wa watoto 8,000 barani Afrika huzaliwa na tatizo hilo na asilimia 15 huhitaji kupandikizwa vifaa hivyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz