Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili kuendesha kambi ya upimaji afya bure

26454 MUHAS+PIC

Sat, 10 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili Muhimbili (MNH) tawi la Mloganzila jijini Dar es Salaam inatarajia kuendesha kambi ya upimaji bure magonjwa  mbalimbali kuanzia Novemba 12 hadi 16.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma MNH, Aminieli Aligaesha jana alisema huduma hiyo itatolewa kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya kisukari.

“Katika kuendelea kutoa huduma kwa wananchi na kurudisha sehemu ya mapato japo kidogo kwa kile kinachokusanywa, Hospitali ya Taifa Muhimbili inawatangazia wananchi kuwa itatoa huduma ya upimaji wa afya bure katika wiki ya kisukari,” alisema.

Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Novemba 14, ambapo mwaka huu inakuja na kauli mbiu isemayo “Familia na kisukari”.

Aminieli alisema katika kuadhimisha siku hiyo Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia tawi la Mloganzila iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo itatoa baadhi ya huduma za uchunguzi bure kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani kwa muda wa siku tano mfululizo.

“Huduma zitakazotolewa ni pamoja na upimaji wa magonjwa ya kisukari, homoni pamoja na shinikizo la damu, uchunguzi wa macho na utoaji miwani kwa watakaobainika kuwa na tatizo, uchunguzi wa afya ya kinywa na meno pamoja na utoaji elimu kuhusu lishe.”

Aligaesha amesema kulingana na kauli mbiu,  wanakaribisha familia kushiriki kuanzia baba mama na watoto na jamii nzima kwa ujumla.

“Ni wajibu wetu ama kuwakinga au kuwatunza wagonjwa wa kisukari walioko katika familia zetu, kuonesha upendo na kushirikiana nao, hivyo nitoe wito kwa wananchi wote watakaopata taarifa hizi kufika katika Hospitali yetu iliyopo Mloganzila,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz