Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili kuendelea kutoa huduma za kibingwa

Muhimbili Kuendelea Kutoa Huduma Za Kibingwa Muhimbili kuendelea kutoa huduma za kibingwa

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Mwaka wa fedha 2023/2024 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepanga kuendelea kutoa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi ikiwemo kuanzisha huduma za kupandikiza mimba, figo, uloto na vifaa vya usikivu Kukamilisha upembuzi yakinifu wa kuimarisha huduma za uchunguzi.

Hayo yamesemwa leo Agosti 10,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof Mohamed Janabi, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za Hospitali hiyo na mwelekeo wa mwaka 2023/24.

Prof Janabi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekamilisha ununuzi wa mashine za kusaidia upandikizaji mimba zilizogharimu Shilingi Bilioni 1.

“Huduma za upandikizaji mimba zitaanza kutolewa hivi karibuni baada ya kamilisha usimikaji wa mitambo ya kutolea hizo,” amesema Prof. Janabi.

Prof. Janabi ameeleza kuwa tatizo la watu kutopata ujauzito ni kubwa na Watanzania wengi wamekuwa wakitoka nje ya nchi kupata huduma za kupandikizwa mimba kwa gharama kubwa hivyo Serikali imesogeza huduma hizo karibu hivyo zitaanza kupatikana hapa hapa nchini.

“Jengo lishakamilika na Muhimbili tulitenga chumba cha kutolea huduma hizo na kwasasa tunasubiri usimikaji wa mitambo hiyo ikamilike ndo tuanze kutoa huduma hizo, na wananchi wanaohitaji huduma hizo hawata kwenda nje ya nchi kupata huduma hizo,” ameeleza Prof. Janabi.

Amesema Kwa kipindi cha mwaka wa fedha uliopita wa 2022&2023 imetoa huduma kwa njia ya msamaha zenye thamani ya TZS 18,264,312,466, sawa na wastani wa TZS 1,522,026,038 kwa mwezi.

Misamaha hii inatokana na vipimo maabara (4%), vipimo radiolojia (0.2%), Dawa (82%), kulala (0.2%), huduma za ICU (0.1%) n.k 7.0 Kuimarika Utendaji wa Huduma Hospitali ya MNH MloganzilaTarehe 03 Oktoba 2018, Serikali iliagiza Hospitali hiyo kuwa chini ya usimamizi na uendeshaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hivyo kwa sasa inaitwa, Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.

Pamoja na hayo amesema jumla ya Wagonjwa 6,200 wanaonwa kwa siku katika Hospitali zote mbili ambapo kwa upande wa Upanga, wagonjwa 3,800 wanahudumiwa kwa siku ikiwa ni wagonjwa wa nje 2,500 na wagonjwa 1,300 ni wagonjwa waliolazwa wodini wakati wote.

Prof.Janabi amesema ,”Muhimbili ikiwa ni Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa na kubwa kuliko zote nchini ina vitanda 2,150 ambapo Upanga kuna vitanda 1,550 na Mloganzila vipo 600 huku Mloganzila ikiwa inahudumia jumla ya wagonjwa 1,400 kwa siku sawa na wagonjwa wa nje 900 na wagonjwa 500 waliolazwa,”amesema.

Kuhusu kupunguza msongamano wa watu Muhimbili, alifafanua kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ilifanya tathimini na kubaini kuwa kwa siku moja eneo hilo wanaingia watu 20,000 na magari 3,500 na kwamba hali hiyo imekuwa changamoto kwani ndugu wa wagonjwa na wafanyakazi walikua wakikosa mahali pa kuegesha magari yao.

“Tathimini hiyo ilionesha kuwa kuna baadhi ya watu wanaegesha magari yao ndani kutokana na usalama uliopo, kutokuwepo mfumo wa malipo ya maegesho ambapo wakishaegesha huenda kufanya shughuli zao Kariakoo au mjini, hali hii ilitulazimu kuanzisha utaratibu wa kulipia huduma ya maegesho ili isaidie kupunguza msongamano wa magari ndani ya Hospitali,”alisema.

Ameongeza kuwa jitihada za kupunguza msongomano Upanga ziligusa pia kuhamisha huduma tatu kwenda Mloganzila kwa lengo lile lile la kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo MNH Upanga na kupunguza idadi ya ndugu wanaokuja kusalimia wagonjwa waliolazwa kutoka watano kwa wakati mmoja hadi wawili asubuhi, mmoja mchana na wawili jioni.

Amesema "uratibu huu unalinda watumiaji wa huduma wakiwemo wagonjwa na wageni wote wanaongia wanaoingia na kutoka ndani ya Hospitali,”amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live