Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muheza yatengewa TSh Bilioni 1.5 kupambana na COVID-19

Muheza Pc Data Muheza yatengewa Sh1.5 bilioni

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo amesema wilaya hiyo imetengewa kiasi cha fedha Sh1.5 Bilioni za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.

Hayo aliyasema wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Bwembela wilayani humo ambapo alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh1.3 trilion zilizotolewa na Serikali hivi karibuni.

Bulembo alisema fedha hizo walizotengewa zinakwenda kumaliza changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madarasa, bweni na madarasa 10 ya shule shikizi na hivyo kufanya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza na wale wa shule shikizi kuondokana na changamoto hiyo.

"Tunaishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kutupatia wana Muheza fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 57, ujenzi wa vituo vitatu vya shule shikizi vyenye madarasa 10, ujenzi bweni moja la wanafunzi wenye mahitaji maalum na ujezi wa vyumba vya huduma za wagonjwa mahututi ( ICU)," alisema Bulembo.

Akitoa mchanganuo wa fedha alisema kwenye ujenzi wa ICU wametengewa Sh100 milioni huku bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum likitengewa Sh 80 milioni.

Kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imepatiwa vyumba 57 vya madarasa kwa Sh20 milioni kwa chumba kimoja hivyo kufikia Sh 1.1 bilioni

Pia katika vyumba vya madarasa vitakavyojengwa katika vituo shikizi vimetengewa Sh200 milioni

Chanzo: mwananchidigital