Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto mwenye kifafa afanyiwa upasuaji wa ubongo Moi kwa saa nne

84355 Kifafa+pic Mtoto mwenye kifafa afanyiwa upasuaji wa ubongo Moi kwa saa nne

Fri, 15 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Madaktari bingwa wa Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Chuo kikuu cha Weill Cornell nchini Marekani kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa ubongo kwa mtoto mwenye kifafa uliofanyika kwa saa nne.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 14, 2019 na mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo,  Dk Respicious Boniface inaeleza kuwa hatua hiyo ni kubwa katika matibabu ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu  nchini.

Amesema  wagonjwa wenye kifafa wanaohitaji upasuaji awali walikua wanapelekwa nje ya nchi na kuigharimu Serikali fedha nyingi.

“Leo ni siku ya nne ya kongamano letu la kimataifa la madaktari bingwa wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, kila mwaka wenzetu hawa kutoka mataifa ya Marekani na Ulaya wamekua wakituletea teknolojia mpya na hii ya upasuaji kwa wagonjwa wenye kifafa ni mojawapo,” amesema Dk Boniface.

Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo wa MOI,  Dk Japhet Ngerageza amesema upasuaji huo umewezekana kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa vilivyonunuliwa na Serikali.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya katika taasisi yetu ya MOI, tunaweza kufanya upasuaji kama huu kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kama EEG, MRI na darubini ya kisasa ya upasuaji wa ubongo ambavyo vyote vimenunuliwa na Serikali,” amesema Dk Ngerageza.

Daktari bingwa wa Ubongo na kifafa kutoka nchini Canada, Dk Evan Lewis amesema ni heshima kuwa sehemu ya kongamano ambalo limesababisha kuanzishwa kwa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wa kifafa Tanzania jambo ambalo litaokoa maisha ya watoto wengi.

Chanzo: mwananchi.co.tz