Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto mwenye jinsi mbili azaliwa Kagera

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Muleba.  Mtoto mwenye jinsi mbili za kike na kiume amezaliwa katika hospitali teule ya Rubya wilayani Muleba mkoani Kagera.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk George Kasibante amesema leo Jumanne Agosti 28, 2018 kuwa mtoto huyo amezaliwa  jana Agosti 27 kwa njia ya kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari na timu ya maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) ofisini kwake, Dk Kasibante amesema uchunguzi wa awali unaendelea kubaini ni kiungo kipi kati ya kike na kiume kinafanya kazi.

"Bado hatujafahamu kiungo chenye nguvu kwa sababu mtoto huyo hajajisaidia haja ndogo tangu alipozaliwa;. Kitaalam bado hatuna wasiwasi labda hadi ikikamilika saa 72 bila mtoto kupata haja ndogo," amesema.

Amesema mtoto huyo atahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza au Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi na huduma zaidi ya madaktari bingwa.

 

Mama mzazi wa mtoto huyo, Flavia Antidius (24) amesema huo ni uzazi wake wa pili na hakuwa na tatizo wakati wa ujauzito na kujifungua.

"Namshukuru Mungu kwa kunijalia kujifungua salama, yote yanayotokea ni mipango yake na kama familia tumeyapokea kwa mikono miwili," amesema Flavia.

Chanzo: mwananchi.co.tz