Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto anaeishi na mvuta sigara hatarini kupata saratani

15895972 1544100512276350 2443343882970984158 O 660x400 Mtoto anaeishi na mvuta sigara hatarini kupata saratani

Thu, 8 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Fransis Furia amesema watoto wanaokaa na watu wanaotumia bidhaa za Tumbaku kama Sigara wako hatarini kupata Saratani.

Dkt. Furia amesema pia, kuna madhara makubwa kwa mtoto aliyeko Tumboni endapo Mama mjamzito atatumia Tumbaku au kukaa karibu na watu wanaotumia bidhaa hizo ikiwemo mtoto kuzaliwa akiwa njiti na kuna uwezekano mkubwa wa mimba kuharibika.

Madhara mengine ni mama kupata Shinikizo la Damu hali ambayo inaweza kusababisha mimba kuharibika. “Tumeshasikia kinamama wakipoteza maisha na nilishawahi kupata kesi ya mama alipoteza mimba 7, lakini yeye hatumii Sigara ila anakaa na mtu anayetumia.

Dkt. Furia amesema uelewa ni mdogo kwa jamii kuhusu madhara ya Sigara kutokana na watu wengi kutokujua sheria kwamba inakataza kuvuta sigara eneo lenye watu.

KIKWETE AIMBIWA HAPPY BIRTHDAY IKULU, RAIS MAGUFULI “MKE WANGU AMEJUAJE BIRTHDAY”

Chanzo: millardayo.com