Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtambo mpya wa saratani kuokoa mabilioni ya fedha

IMG 20210712 205459 686 Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtambo mpya utakaofungwa mwezi Juni mwaka 2022 kwa kubaini ugonjwa wa saratani na kemia unatarajiwa kuokoa zaidi ya Tsh. bilioni 5 zilizokuwa zikitumika kupeleka wagonjwa nje kwaajili ya kufanyiwa vipimo.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, wakati akijibu hoja za wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii walipofanya ziara ya kutembelea mradi huo unaojengwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).

Alisema baada ya kukamilika kwa mradi huo Juni mwaka huu fursa iliyoko ni kuwatibu wagonjwa ambao walikuwa wanawapeleka nje ya nchi kufanya kipimo hicho na kutumia Sh. bilioni 5 kwa kila mwaka.

“Sasa tunakwenda kuokoa hii Sh. bilioni 5 ambayo ilikuwa inatumika huko nje ya nchi na pia tutauza mionzi kwa nchi nyingine ambapo za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa nchi zinazotuzunguka zitakuja kununua miozi hapa nchini,” alisema.

Alisema fedha hizo zitatumika kufanya matibabu kwa mwananchi mnyonge ambaye anatabiwa bila gharama.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage, alisema wataalamu wakiwamo madaktari bingwa watatu kwa ajili ya kutoa huduma hizo mpya za mashine ya PET/CT Scan.

Alisema gharama za kipimo hicho ni Sh. milioni 1.6 kwa mgonjwa mmoja na taratibu zinaendelea za kupata gharama halisi mradi utakapoanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live