Mikoani. Ikiwa imebaki siku moja kumalizika kwa kampeni ya chanjo ya maradhi ya surua , rubela na polio kwa watoto wenye umri wa miezi tisa hadi 59, wazazi na walezi mkoani Geita wameshauriwa kutumia muda uliobaki kuhakikisha watoto wenye sifa wanapata chanjo
Mratibu wa chanjo mkoani hapa, Wille Luhangija amesema mwitikio sio wa kuridhisha kwani kwa siku tatu wametoa chanjo kwa watoto 198,929 sawa na asilimia 48 ya walengwa 413,875 waliotarajiwa .
Akizungumzia chanjo ya polio ya sindano, Luhangija amesema hadi kufikia oktoba 19 mwaka huu ni watoto198,087 sawa na asilimia 60 ya walengwa 171,325 wanaotakiwa kupewa chanjo hiyo .
“Chanjo ni zawadi kwa maisha ya mtoto zinatolewa bila malipo na nisalama kwa watoto nawaomba san asana tuwakinge watoto dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo”amesema Luhangija.
Luhangija amesema Chanjo hiyo imethibitishwa na shirika la afya ulimwenguni na shirika la ubora wa vyakula duniani pamoja na wizara ya afya nchini kuwa ni salama kwa maisha ya binadamu hivyo kuwataka wazazi na walezi kujitokeza kuwapeleka watoto ili wapate kinga.
Baadhi ya wazazi, Izack Magesa aliyempeleka mtoto kwenye chanjo ameliambia Mwananchi kuwa kampeleka mwanawe ili aweze kupata chanjo na kumkinga na maradhi yanayoepukika huku akiwataka wanaume kujenga utamaduni wa kuwapeleka watoto wao na sio kuwaachia wanawake tu.
Pia Soma
- Kuolewa kunavyowatatiza wanawake nchini
- Mkanganyiko wizi wa kompyuta ofisi za DPP
- Msanii Harmonize azindua mgahawa wa KondeBoy, kugawa vyakula miezi sita