Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wa pili chanjo Corona wazinduliwa

64dc36490bc266f8696e126d2ab9c092 Mpango wa pili chanjo Corona wazinduliwa

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali, inatarajia kuchanja chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona (Covid-19), kwa wananchi 80,000 hadi 100,000 kwa siku, kupitia mpango wake wa harakishi na shirikishi kwa jamii awamu ya pili, dhidi ya janga hilo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi, katika uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, jijini Arusha leo umesema mpango huo una lengo la kufikia kuchanja wananchi 80,000 mpaka 100,000 kwa siku.

“Huu mpango unatuondoa kwenye kuchanja watu 20,000, 30,000 na 40,000, unatupeleka kwenda kuchanja watu 80,000 hadi 100,000 kwa siku moja,” amesema Profesa Abel Makubi.

Katibu mkuu huyo wa Wizara ya afya, amesema kila mkoa utatakiwa kuchanja wananchi kuanzia 4,000 hadi 5,000 kwa siku, ili baada ya miaka miwili asilimia 60 ya watu wawe wamepata kinga hiyo dhidi ya Covid -19.

Profesa Makubi, amesema, ili lengo hilo liweze fanikiwa, serikali imeongeza vituo vya utoaji chanjo.

“Tunaongeza vituo kutoka 6,784 viwe zaidi ya 7,000 hadi 8,000. Pamoja na kuweka sehemu za kuchanja kwenye mitaa, hawa wahudumu katika ngazi ya jamii watakuwa kwenye mitaa mbalimbali kuweka mahema, vituo na hata kwenye nyumba hadi nyumba, kuelimisha wananchi waweze kuchanja,” amesema Profesa. Makubi.

Amesema, hadi kufikia tarehe 18 Desemba 2021, Serikali imepokea dozi milioni 4.4 za chanjo ya Covid -19, ikiwemo aina ya Pfizer na Sinopharm.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live