Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango uwekezaji afya mama na mtoto wazinduliwa

Othman Mpango uwekezaji afya mama na mtoto wazinduliwa

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman amezindua Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto Tanzania wa miaka mitano unaofadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Global Financing Facility wenye lengo la kuimarisha afya ya mama na mtoto.

Akizundua Mpango huo Othman amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya na kuweza kuzindua mpango wa uwekezaji katika afya ya mama na mtoto ambao unalenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya nchini.

Amesema mpango huo utatekelezwa chini ya usimamizi wa wizara ya Afya Tanzania Bara, wizara ya Afya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo uwekezaji wake utagharimu Dola Milioni 275 za Kimarekani ambapo Dola Milioni 250 za Kimarekani ni mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia na Dola Milioni 25 ni kutoka Global Financing facility.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Godwin Mollel amewataka Wataalamu kuhakikisha sehemu ya fedha hizo inaelekezwa kwenye eneo la lishe katika kipindi cha ujauzito na baada ya mama kujifungua ili kupata watoto wenye uwezo mkubwa kiakili na afya bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live