Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango jumuishi wa lishe watekelezwa kwa 80%

Jenista (1) Jenista Muhagama, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, bunge, kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewataka watendaji wanaohusika na afua za lishe nchini kusimamia vema taratibu za upatikanaji na ulaji wa lishe bora ili kujenga taifa imara na lenye nguvu.

Waziri Jenista ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati alipokua akitoa taarifa ya mpango jumuishi wa kwanza wa lishe ulioanza rasmi nchini kwenye mwaka wa fedha 2014/ 2015.

Amesema swala la lishe ni swala linalotakiwa kupewa kipaumbele kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa lengo likiwa ni kutoa makuzi bora ili kuepuka udumavu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live