Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wa kibatari wasababisha vifo vya watoto wawili

10508 Moto+pic TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Muleba.Watoto wawili wa kike wamefariki  dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Agosti 7 katika katika kijiji cha Rwazi kata ya Kikuku, Kagera.

Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni  kibatari kilichokuwa kikiwaka, kuangukia godoro na chandarua.

Mwenyekiti wa kijiji cha Rwazi wilayani Muleba Wilbard Kagombora amesema wakati moto huo unashika, mama wa watoto hao  alikuwa  amekwenda kwa jirani kuomba chumvi.

Kagombora amesema tukio hilo limetokea jana saa 2 usiku.

“Mtoto mmoja  ana umri wa miaka miwili na mwingine ana miezi sita,”amesema.

"Ndugu yao  mwenye miaka minne alipiga kelele lakini mama yao alipofika  alikuta nyumba imezingirwa moshi na moto mkali na kushindwa kuingia hadi ulipopungua na walipofanikiwa kuingia ndani waliwakuta watoto hao wakiwa wameteketea" ameongeza:

Amesema nyumba hiyo ilijengwa kwa tofali za udongo na kuezekwa bati lakini ndani  vyumba vyote vilisambazwa nyasi za kukalia  hali iliyosababisha moto kusambaa kwa kasi.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Agustino Ollomi amesema amepokea taarifa hizo na akatoa  rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz