Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Mother’s Day’ Boomplay Yafanya Jambo Hospitali Ya Mwananyamala

Boom Play 3?fit=700%2C394&ssl=1 ‘Mother’s Day’ Boomplay Yafanya Jambo Hospitali Ya Mwananyamala

Mon, 10 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

‘Mother’s Day’ Boomplay Yafanya Jambo Hospitali Ya Mwananyamala May 10, 2021 by Global Publishers



Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (kulia) akiwashukuru wauguzi wa hospitali ya Mwananyamala mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba katika hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.

App ya Boomplay inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki imeadhimisha Siku ya Akina Mama (Mother’s Day) mwaka huu kwa kutoa vifaa vya matibabu kwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo katika kuboresha afya salama na ya uhakika kwa akina mama nchini.



Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Muuguzi Kiongozi Idara ya nje ya Hospitali ya Mwananyamala, Henrietta Ishara (wa tano kulia).

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la hospitali hiyo, Jumapili Mei 9,2021, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli amsema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mipango endelevu inayolenga kusaidia jamii.

“Tunayo furaha kuitumikia jamii yetu na hasa katika siku hii ya akina mama duniani. Tunaelewa mchango na shida wanazopitia akina mama hasa wakati wa uzazi katika jamii zetu. Tunapowasherehekea akina mama, tunafurahi kuchangia msaada wetu na tunatarajia kufanya mengi zaidi kwenye jamii katika siku usoni,” alisema Stambuli.



Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Muuguzi Kiongozi Idara ya nje ya Hospitali ya Mwananyamala, Pendaeli Massay (mwenye gauni la bluu).

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Zavery Benela, aliisifu kampuni hiyo kwa msaada wake, na kuongeza kuwa umekuja katika muda muafaka wakati ambao ulimwengu unakabiliwa na changamoto ya huduma ya afya.

“Kwa niaba ya hospitali nzima, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Boomplay kwa msaada huu wa huruma. Tuna hakika kuwa mchango wao utasaidia sana katika kuhakikisha huduma zetu za kina mama zinaendelea bila kukatizwa,” alisema Dkt. Zavery Benela.
Chanzo: globalpublishers.co.tz