Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mollel awasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza stoo Ngara (+video)

Video Archive
Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Godwin Mollel, amewasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza Stoo wa Hospitali ya Wilaya ya Ngara ya Nyamiaga mkoani Kagera ili kupisha uchuguzi.

Watumishi hao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na upotevu wa dawa za mamilioni ya fedha zilizoletwa na Serikali kwa ajili ya wananchi.

Akizungumza na Watumishi wa Afya wilayani humo juzi, Dk. Mollel amesema Serikali chini ya Rais Dk. John Magufuli, haiwezi kuvumilia watumishi wasio waadilifu wanaoiibia serikali kwa manufaa yao binafsi hivyo ni lazima wakae pembeni kwanza wakati uchunguzi wa tuhuma zao ukiendelea na itakapobainika wamehusika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO), Revocatus Ndyekubora, Mfamasia wa Hospitali, Patrick Ogo na Mtunza Stoo, Gaston Bakulu, kwa tuhuma za kujihusha na utoroshaji wa dawa ya hospitali na kuziuza kwa wafanyabiashara.

Amesema watumishi hao wamekuwa wakishiriki kuihujumu serikali huku hosipitali, vituo vya afya na zahanati vikikosa madawa na wagonjwa kuhangaika kupata huduma wanapoenda kutibiwa.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Aidan Bahama, kuwatafutia kazi nyingine watumishi.

“Serikali haiwezi kuwavumila watumishi wasio waadilifu, hili ni fundisho kwa watumishi wengine wanaotumia vibaya mali za umma, tutawaondoa,” Dk. Mollel.

Chanzo: millardayo.com