Tue, 12 Mar 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amewataka wahudumu sekta ya afya kutanguliza maslahi ya nchi mbele pamoja na ya Watanzania wanaowahudumia.
Dk. Mollel ameyasema hayo kufuatia video iliyoko mtandaoni ikionyesha baadhi ya hospitali za Serikali na Binafsi zikisambaza baadhi ya dawa ambazo wanadai hazipo kwenye kitita cha bima ya afya.
Dk. Mollel amesema kuwa kitita hicho kimezingatia muongozo wa dawa muhimu katika nchi na kusema kuwa kama serikali inaendelea kupokea mawazo ya nini kiboreshwe katika kitita hicho na kuwahikikishia Watanzania kuwa hakuna mwananchi atakayekosa dawa.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live