Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moi yawakumbuka watoto wenye vichwa vikubwa, mgongo wazi

Dabecfdc1013ed8d0014ad3a3fde9a1d Moi yawakumbuka watoto wenye vichwa vikubwa, mgongo wazi

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Mifupa ya MOI imesema katika kuadhimisha miaka 23 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, kesho Septemba 11,2020 itafanya upasuaji kwa watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa kwa wale watakaokuwa wamefika Hospitalini hapo.

Sababu kubwa ya watoto kuzaliwa na mgongo wazi na vichwa vikubwa ni ni ukosefu wa madini ya folic acid na hivyo wataalamu wa afya wanaeleza kuwa wanawake wenye umri wa kuzaa wameshauriwa kula vyakula vyenye folic acid zikiwemo mboga za majani na matunda ili kuwaepusha na matatizo ya kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Ingawa watoto wanaozaliwa na matatizo haya wanatoka sehemu mbalimbali nchini, lakini takwimu zinaonyesha wagonjwa wengi wanatokea katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Mwanza.

Mbali na tatizo la lishe, Dk. Marks Mwandosi ambae ni mtaalamu wa upasuaji katika hospitali ya Muhimbili aliwahi kukaririwa akisema kuwa mtoto pia anaweza kuzaliwa katika ule mfumo wake wa maji ya kwenye ubongo ambayo yanalinda ubongo, yakawa hayazunguki katika mfumo wa kawaida. Hii inatokana na mtoto jinsi alivyoumbwa tumboni. Inawezekana ikawa kuna kuzibwa au yakawa hayanyonywi vizuri au yanatengenezwa mengi.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya afya, tatizo la kujifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi linaepukika. Kinachotakiwa kwa kina mama wajawazito ni kupewa uelewa wa kutosha kuhusu lishe hasa katika kipindi cha ujauzito.

Chanzo: habarileo.co.tz