Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moi yaanza Uchungunzi wa Ubongo bila kufungua fuvu la kichwa

Def48a5eef05524199cc06a7e409a98c Moi yaanza Uchungunzi wa Ubongo bila kufungua fuvu la kichwa

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Mifupa Muhimbili(MOI) kwa mara ya kwanza imeanza kutoa huduma ya uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu la kichwa.

Uchunguzi huo umefanywa kwa saa tatu katika maabara ya kisasa ya upasuaji wa ubongo na jopo la madaktari bingwa, wauguzi, watalamu wa radiolojia wazalendo sita kutoka MOI, Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete(JKCI) pamoja na Hospitali ya Agakhan.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface amesema kuanza kwa maabara hiyo ni ishara ya mageuzi makubwa katika sekta ya afya hapa nchini kwani maabara kama hiyo haipo kwenye nchi nyingine kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Leo ni siku ya furaha sana kwani tumeanza kutumia maabara yetu ya upasuaji wa ubongo, hii imewezekana kutokana na dhamira ya dhati ya Rais John Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini kwani maabara hii imejengwa Serikali ya awamu ya Tano kwa zaidi ya Sh bilioni 7.9,”alisema Dk Boniface

Chanzo: habarileo.co.tz