Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mochwari ya Muhimbili unaweza kunywa chai - Prof. Janabi

Profesa Janabi Muhimbili A06091 Mochwari ya Muhimbili unaweza kunywa chai - Prof. Janabi

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya kudumu ya Bunge la Afya na Ukimwi jana Feb 22,2024 imetembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kukagua maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi.

Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na kamati hiyo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Dkt. Faustine Ndugulile ni pamoja na eneo la kuhifadhia Maiti ( Monchwari) ambapo kamati imeonyesha kuridhishwa na ununuzi wa Majokofu ya kisasa ya kuhifadhia Maiti kwa kutumia fedha za ndani badala ya kusubiri fedha kutoka Serikali kuu.

Prof. Mohamed Janabi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospital hiyo amesema kutokana na majokofu 76 yaliyokuwepo hapo awali kukaa muda mrefu na nguvu yake ya kutunza Miili kupungua kama Taasisi waliamua kutumia fedha za ndani walizo kusanya ,ambapo Ununuzi wa Majokofu hayo 99 walionunua Afrika Kusini yamegaharimu Bilion 1.6.

Katika hatua nyingine Prof Janabi amesema kama Hospital ya Muhimbili kwa Mwaka Jana walitoa msamaha wa Bilion 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live