Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MoI kuchunguza umri kwa kutumia kiganja cha mkono

10631 Moi+pic TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MoI) imeanza kuendesha uchunguzi wa kubaini umri wa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 ili kubaini kama kuna hali yoyote ya udanganyifu.

Uchunguzi huo unafanywa na wataalamu wa Radiolojia kwa kutumia kipimo kifahamikacho kama MRI.

Akizungumza leo Agosti 7, Mkurugenzi Mtendaji wa MoI Dk Respicious Boniface amesema taasisi hiyo imechaguliwa kuwa kitovu cha kufanya uchunguzi huo kutokana na kuwa na vifaa vinavyokidhi vigezo vya kimataifa.

"Vijana hawa watafanyiwa uchunguzi kwenye kituo chetu na vijana 25 watafanyiwa uchunguzi huo," amesema.

Amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kupima kiganja cha mkono wa kushoto ambacho kinaweza kutoa usahihi wa umri wa kijana.

Vijana hao walio chini ya umri wa miaka 17 watashiriki michuano  ya Baraza la Vyama vya michezo ya Afrika Mashariki na kati. 

Michuano hiyo itaanza mwishoni mwa wiki katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz