Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

 Mmoja afariki, nane taabani kwa kula mzoga wa 'kitimoto' pori

F02c028a18cc2968ecc98c02a3814df2  Mmoja afariki, nane taabani kwa kula mzoga wa 'kitimoto' pori

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine nane wamelazwa katika kituo cha afya cha Mishano kilichopo wilayani Tanganyika, mkoani Katavi baada ya kula nyama inayosadikika kuwa ni ya nguruwe pori.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa waathirika katika tukio hilo walikuta mzoga wa mnyama huyo ukiwa jirani na mashamba yao na kugawana nyama yake kwa ajili ya kitoweo.

Kamanda alimtaja aliyekufa kwenye tukio hilo kuwa ni Katarina Zebedayo.

“Inadaiwa baada ya kutumia kitoweo hicho na kupata madhara walianza kutumia dawa za kienyeji hadi mmoja wao alipofariki ndipo Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Theodoli Philipo alibaini na kufanya jitihada za kuwafikisha katika kituo hicho cha afya,” amesema Kuzaga.

Chanzo: habarileo.co.tz