Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mloganzila yawarejeshea matumaini watoto watatu wenye matatizo ya kusikia

82813 PIC+MLO Mloganzila yawarejeshea matumaini watoto watatu wenye matatizo ya kusikia

Tue, 5 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Upasuaji na upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto watatu wenye waliokuwa na matatizo ya kusikia umefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya leo vifaa hivyo kuwashwa.

Watoto watatu akiwemo mmoja raia wa Rwanda  walifanyiwa upasuaji huo Oktoba 3 na 4 mwaka huu katika hospitali ya Mloganzila.

Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya masikio, pua na koo hospitalini hapo, Godlove Mfuko amesema watoto walikuwa wakifuatiliwa kwa mwezi mzima hadi ulipofika wakati wa kuwashiwa vifaa hivyo.

“Baada ya kuwafanyia upasuaji huwa tunaka muda kama wa mwezi mmoja kwaajili ya kuwasha kifaa hicho ambacho kitamwezesha kusikia na wanaonekana kuendelea vizuri,”

Amesema kwa sasa hospitali hiyo imejiwekea lengo la kufanya upasuaji wa aina hiyo kwa watoto 24 kwa mwaka.

Raphaeli  Kapande ambaye ni mzazi wa miongoni mwa watoto waliopandikizwa kifaa hicho  ameishukuru serikali na madaktari waliomwezesha mwanae kufanyiwa upasuaji na kuwashiwa kifaa hicho. "Nilikuwa napata sana shida kuwasiliana na mwanangu lakini baada ya kuwashiwa kifaa hiki nashukuru anaweza kusikia na kuelewa ninachomweleza" amesema Kapande.

Mzazi mwingine Laurencia Chaula mkazi wa kigamboni  amesema amepata matumaini ya kuanza kufanya mawasiliano na mtoto wake jambo ambalo amelikosa kwa muda mrefu.

"Nlikuwa nikiwasiliana na mwanangu kwa njia ya ishara lakini baada ya kuwashiwa kifa hiki itaniwezesha kuwasiliana nae kawaida"alisema Chaula

Chanzo: mwananchi.co.tz