Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwasa arejea nchini na afya njema

12944 Pic+mkwasa TanzaniaWeb

Tue, 21 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Katibu wa Yanga, Boniface Mkwasa amerejea nchini akitokea katika matibabu ya moyo nchini India, na kusema angalau kwa sasa hali yake imeimalika.

Akizungumza mara baada ya kutua Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkwasa alisema hali yake ilikuwa mbaya, lakini anashukuru Mungu kwa upasuaji aliofanyiwa umefanya hali yake kurejea.

"Baada ya vipimo ndipo nilipobaini nilikuwa na tatizo kubwa ambalo lingefanya nifie mazoezini ama usingizini, nashukuru sana familia yangu hasa mke wangu Betty kushikamana nami kuanzia mwanzo mpaka hii leo.

"Pia nashukuru TFF kwa msaada wao wa hali na mali bila kuwasahau Watanzania wote walioniombea ili nipone," alisema Mkwasa.

Mke wake Betty Mkwasa alisema madaktari wamwaambia mume wake anatakiwa kupumzika miezi mitatu bila kufanya kazi ngumu na kisha watatakiwa kurejea India ili kujua nini kitafuata.

"Baada ya miezi mitatu tutarejea tena India ili madaktari wakajue maendeleo yake, hivyo niwashukuru wote waliotuunga mkono" alisema Betty.

Chanzo: mwananchi.co.tz