Arusha. Mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kujadili ugonjwa wa corona umekwama kufanyika leo Jumatano Aprili 15, 2020.
Mkutano huo ulikuwa ufanyike kwa njia ya video ukiwahusisha marais wa nchi sita wanachama wa jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Burundi na Rwanda.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Balozi Liberat Mfumukeko ametoa taarifa hiyo leo akibainisha kuwa kukwama kwa mkutano huo kumetokana na
na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir kuwa na majukumu mengine.
"Sudan Kusini hivi karibuni wameunda Serikali ya mseto hivyo bado wanajipanga na kwa mujibu wa mkataba wa jumuiya mkutano hauwezi kufanyika kama nchi moja haipo," amesema
Hata hivyo, mkutano wa mawaziri wa afya ulifanyika na kuelezwa kuwa kila nchi inaendelea vizuri katika mapambano dhidi ya corona.
Habari zinazohusiana na hii
- Bila barakoa hakuna kuingia KCMC
- EAC yatoa ‘maabara zinazotembea’ kwa nchi wanachama kupima virusi vya corona
"EAC tunaendelea kushirikiana na nchi wanachama kuhakikisha tunapambana na ugonjwa huu kwa kupunguza maambukizi zaidi na kufanikisha matibabu na kinga,” amesema.
Leo ni mara ya tatu mkutano huo unaahirishwa kutokana na mmoja wa viongozi kukosekana kwa sababu ya kukabiliwa na majukumu mengine.