Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi wa wizara ya Afya awapigia magoti mabalozi

11749 Magoti+pic TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kitengo cha familia, Wizara ya Afya, Grace Mwangwa, amewapigia magoti mabalozi wa nchi mbalimbali akiwaomba kuunga mkono juhudi za Tanzania katika kupambana na vitendo vya ukeketaji.

Mangwe alifanya kitendo hicho katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya ukeketaji iliyopewa jina la ‘In the Name of Your Daughter’.

Filamu hiyo imeongozwa na Giselle Portenier, mwandishi wa habari wa Canada, aliyejikita katika masuala ya haki za binadamu kwa wanawake na watoto.

Walioshiriki katika utayarishaji wa filamu hiyo ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani   (UNFPA), Umoja Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC).

Wengine ni ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Ireland, Ubalozi wa Uholanzi, pamoja na ubalozi wa Canada.

Mabalozi waliokuwepo katika hafla hiyo ni  wa EU, Roelandf  Van de Geer,  Balozi wa Uingereza  Sara Cooke na Balozi wa Ireland, Paul Sherlock ambao wote kwa nyakati tofauti walionyesha nia kuunga kampeni hiyo.

Wakati anasoma hotuba yake, Mangwe aliomba radhi na kuikatisha, kisha akasogea pembeni na kupiga magoti akisema:

“Kwa heshima yenu mabalozi tunaomba mtusaidie katika mapambano haya ya ukeketaji kwa watoto wetu kwani vitendo hivyo vimekuwa na athari kubwa katika jamii ikiwamo kusababisha vifo, kwa ushirikiano wenu pamoja tutaweza.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake(Tamwa), waandaaji wa tukio hilo kupitia Mkurugenzi wao, Edda Sanga, alisema filamu hiyo imeigizwa na watoto walio katika nyumba salama, ambayo huifadhi watoto wanaokimbia vitendo vya ukeketaji.

“Ni filamu yenye mafunzo mengi na anaamini itagusa nyoyo za watu, kwani imeshirikisha wasanii ambao wamepitia matatizo hayo na wanachokiongea wana ushahidi nacho,”amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz