Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkunga asema kifafa cha mimba kinaweza kutibika

7e8c881e7dbd72473a6f7b532ec2107a Mkunga asema kifafa cha mimba kinaweza kutibika

Mon, 9 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MUUGUZI Mkunga wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Paul Sanka amesema kifafa cha mimba kinaweza kuzuilika endapo mjamzito atawahi kliniki.

Akizungumza na HabariLEO, Dk Sanka alisema kifafa cha mimba kwa wajawazito kwa sasa kimekuwa changamoto kubwa, hivyo ni muhimu akinamama wakahudhuria kliniki mapema kabla ya madhara hayajajitokeza.

Alisema kifafa cha mimba kwa wajawazito ni hatari kwani husababisha vifo au ulemavu wa kudumu.

Dk Sanka aliwashauri wajawazito pamoja na wenza wao kuwahi kliniki mapema ili kubaini dalili za ugonjwa huo na kuzuia madhara mbalimbali wanayoweza kupata mama na mtoto katika kipindi cha kujifungua.

Mtaalamu huyo aliwataka akinamama kujiunga na huduma za uzazi wa mpango kwa makubalino na wenza wao, ili kupanga idadi ya watoto wawatakao kwa wakati sahihi.

Alisema kwa sasa idadi ya vifo vya akinamama na watoto imepungua tofauti na hali ilivyokuwa na kwamba, hali hiyo inatokana na huduma za afya zilizoboreshwa.

Kwa mujibu wa Dk Sanka, kutokana na baadhi ya watu kushindwa kukubaliana na matumizi ya njia za uzazi wa mpango, baadhi ya wanawake wamekuwa wakipata ujauzito bila kutarajiwa hali inayowafanya wengine kufanya uamuzi mbaya kwa kisingizo kuwa mimba ilipatikana kwa bahati mbaya jambo alilosema siyo kweli.

Chanzo: habarileo.co.tz