Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkoa wa Kilimanjaro wapokea magari 15 ya sekta ya afya

Mkoa Wa Kilimanjaro Wapokea Magari 15 Ya Sekta Ya Afya.jpeg Mkoa wa Kilimanjaro wapokea magari 15 ya sekta ya afya

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Kilimanjaro umepokea jumla ya magari 15 katika Sekta ya Afya kati ya hayo magari 10 ni ya kubebea wagonjwa (Ambulance), na magari 5 ni kwa ajili ya utawala ambayo yatatumika kwenye huduma za usimamizi shirikishi na usabazaji chanjo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ambapo alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya mapinduzi makubwa na uwekezaji katika miradi ya Maendeleo hususani sekta ya Afya.

Babu alisema kuwa, lengo la kuborsha sekta ya afya ni kuhakikisha Makundi yote kwenye jamii yanapata huduma za afya bora na zenye viwango vinavyotakiwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025.

“Magari haya ymepatikana kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya bora na zenye viwango hivyo magari haya yatumike kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo” alisema Babu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live