Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkapa akumbukwa kwa kuboresha afya

Ripp Ed Mkapa akumbukwa kwa kuboresha afya

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Walitoa maoni hayo jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara, ikiwa zimebaki siku chache kuadhimisha kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo chake. Mkapa alifariki dunia Julai, mwaka jana.

Akizungumza na Nipashe, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Frolian Tinuga, alisema Mkapa alikuwa na maono katika kusaidia sekta ya afya ndiyo maana alianzisha BMF kwa lengo la kusaidia Watanzania.

BMF, alisema tangu kuanzishwa kwake,  imesaidai upatikanaji wa watumishi 128  wa sekta ya afya mkoani Mara.

Dk. Tinuga alisema licha ya kuwezesha upatikanaji wa watumishi, pia kuna wataalamu waliosomeshwa na BMF na kuajiriwa sekta binafsi na serikalini katika sekta ya afya nchini.

Aliongeza kuwa Mkapa alitumia muda wake baada ya kustaafu kuhakikisha taasisi yake inajikita kusaidia jamii kupunguza uhaba wa watumishi na upatikanaji wa huduma bora za afya.

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murangi, Dk. Yusuph Wambura, alisema maono ya hayati Mkapa yamesaidia  kuboresha huduma za afya.

Alisema kabla ya kuwapo BMF, walikuwa na uhaba wa watumishi sekta ya afya hususani upande wa upasuaji lakini kwa sasa wanahudumia wanawake 150 hadi 160 wanaojifungua kwa mwezi na kwa siku wanahudumia wagonjwa wa nje kati ya 50 na 70 kwa siku.

Pia Dk. Wambura alisema kituo hicho kina uwezo wa kulaza wagonjwa 25 hadi 30 wanaotoka kata 16.

Alisema alisema mpaka sasa wamesaidiwa watumishi zaidi ya 10 akiwamo daktari wa dawa za usingizi pamoja na wauguzi.

Akizungumzia huduma za afya, Mratibu wa BMF Kanda ya Ziwa, Dk. Remmy Moshi, alisema taasisi hiyo imekuwa msaada kwa kutoa watumishi katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Alisema BMF imewezesha upatikanaji wa watumishi 128 wa taaluma tofauti katika sekta ya afya.

Pia alisema BMF imekuwa na jukumu la kuziba nafasi mbalimbali ambazo kuna uhaba wa watumishi na kwamba jambo hilo limefanikiwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Chanzo: ippmedia.com