Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitindo ya maisha huchangia magonjwa ya Moyo, Saratani, Figo na Presha - Dk. Kiholongwe

WhatsApp Image 2021 11 10 At 5.30.39 AM.jpeg Epukeni mitindo ya maisha yenye athari za afya - Dk. Kiholongwe

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeitaka jamii kuachana na mtindo usiofaa wa Maisha ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza Dkt. James Kiholongwe wakati akitoa elimu kwenye wiki ya kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ambapo amesema kuna kila sababu ya jamii kujizuia kuishi maisha yanayoweza kuathiri afya zao.

Dkt. Kiholongwe amesema kuwa, watu wengi ambao wana matumizi ya pombe, uvutaji wa sigara, matumizi ya vyakula vyenye mafuta na kutokufanya mazoezi wamejikuta kwenye wimbi la kupata magonjwa yasiyoambukiza hivyo kuathiri nguvu kazi ya Taifa.

Dkt. Kiholongwe ameyataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni pamoja na kisukari, ugonjwa wa moyo, saratani, figo na shinikizo la damu ambayo vichocheo vikubwa ni kuishi mtindo wa maisha usiofaa usioendana na ulaji wa vyakula na vinywaji vinavyotakiwa.

Katika hatua nyingine Dkt. Kiholongwe ameitaka jamii kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi na kupima afya mara kwa mara Ili kujua mwenendo wa afya kwani itasaidia kujiepusha na magonjwa hayo.

Wizara ya Afya inaadhimisha wiki ya Kitaifa ya kuzuia na kudhibiti  magonjwa yasiyoambukiza yenye kauli mbiu "Badili Mtindo wa Maisha,Boresha Afya" kuanzia Novemba 06 hadi 13 kila mwaka na mwaka huu yanafanyika jijini Arusha na katika kuhitimisha maadhimisho hayo mgeni rasmi atatarajiwa kuwa Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima.

Chanzo: ippmedia.com