Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miradi ya Afya chini ya mpango IMF kukamilika kabla ya Juni 30

Prof Mabel.jpeg Miradi hiyo inatekelezwa kwa fedha za mkopo toka IMF

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameagiza miradi yote ya Wizara ya Afya chini ya Mfuko wa fedha wa kimataifa (IMF) iwe imekamilika kabla ya mwezi June 30, 2022.

Ameyasema hayo Tarehe 20 machi, 2022 mkoani Ruvuma alipotembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa huo,

"Naagiza nchi nzima miradi yote ya IMF kwenye sekta ya afya inayosimamiwa na wizara ya afya iwe imesha kamilika tarehe 30 june 2022 , nje ya hapo ni kukaidi maagizo ya Viongozi na masharti ya matumizi ya Fedha hizi na tutakuondoa"

Aidha Prof Makubi amewataka uongozi wa Hospitali ya mkoa wa Ruvuma kukaa na mkandarasi , ofisi ya Katibu Tawala Mkoa, Mshauri elekezi na Watalaamu wa Majengo toka wizara ya Afya kuhakikisha mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kabla ya mwezi wa sita kuisha,

"Kakaeni pamoja, ule mradi watu wafanye masaa ishirini na nne , mkandarasi aongeze wafanyakazi , waweke taa za usiku wafanye kazi usiku na mchana ili wakabidhi kabla ya mwezi wa sita haujaisha" amesema Prof Makubi

Kwa upande mwingine Prof Makubi amewapongeza uongozi wa Hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa kufanya vizuri kitaifa katika eneo la chanjo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO -19

Chanzo: www.tanzaniaweb.live