Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa yeye sio mbaguzi lakini jambo la kukusanya fedha kwa watu maskini alafu fedha hizo zinapelekwa kwa wawekezaji wa nje ni jambo ambalo linauma. Rais Magufuli ameyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD).