Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mifupa yangu imeoza miaka 10 sitembei, nimeenda kwa waganga 7 sijapona”

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: --

Bi. Celina Nikodem Mkazi wa Mlole Mkoani Kigoma anaomba msaada wa matibabu au kupata Baiskeli (Wheelchair), hii ni baada ya kupooza miguu tangu mwaka 2009 na hivi sasa ni takribani miaka kumi hajawahi kutembea wala kusimama.

Bi. Celina anasema alikwenda Hospitali Kigoma na kuambiwa mifupa ya mwilini mwake imeoza na akapewa dawa ambazo alitumia kwa muda mrefu bila ya mafanikio ndipo alichukua uamuzi wa kwenda kwa Waganga wa kienyeji zaidi ya 7 na bado hakupata nafuu.

Kwa sasa Bi.Celina hajiwezi kwa lolote kila kitu anafanyiwa na Binti yake ambae amamfulia nguo,kumuogesha, kumpikia, Kumbadilisha nguo pamoja na kutafuta chakula kwa ajili ya familia

Chanzo: --