Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka mitano mapinduzi ya tiba kupitia mionzi ya nyuklia

78622 Pic+vipimo

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wataalamu wa vipimo vya mionzi ya nyuklia nchini Tanzania wamesema uwepo wa mashine hizo kwa kipindi cha miaka mitano, imewezesha utambuzi wa mapema wa magonjwa na matibabu sahihi kwa mgonjwa.

Wataalamu hao kutoka Hospitali ya Aga Khan, Ocean Road na Bugando, wamesema mashine hizo zimeweza kusaidia pia kugundua mapema magonjwa ya saratani, moyo na figo ikilinganishwa na CT Scan kwa kuwa zina uwezo wa kuona ndani ya chembe chembe za mwili.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya huduma za nyuklia yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 6 hadi 12, 2019.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 Mkurugenzi wa tiba hospitali ya Aga Khan Dk Ahmed Jusabani amesema wakati hospitali hiyo ikisherehekea miaka mitano ya utoaji huduma kupitia mashine hiyo, wameweza kufanikiwa kutibu zaidi ya wagonjwa 800 ambao walipimwa na kugundulika na matatizo ya magonjwa mbalimbali kupitia kipimo hicho.

“Asilimia 99 ya magonjwa yaliyogundulika ni pamoja na yale ya moyo, figo, saratani, mifupa, uvimbe pia. Tumeanzisha mashine nyingi lakini changamoto kubwa bado watoa huduma wengi hawajajua umuhimu wa mashine hizi ndiyo maana tumetoa mafunzo kwa watoa huduma nchini ili kufikisha elimu kwa wataalamu na wananchi wa kawaida,” amesema Dk Jusabani 

Mwezeshaji mafunzo wa mashine za nyuklia kutoka Kampuni ya Siemens Dk Viola Satzinger amesema amekuja katika ukanda wa Afrika Mashariki lengo ni kuwezesha wataalamu wa afya kujua umuhimu wa kutumia kipimo hiki kwa wagonjwa ili waweze kutoa matibabu sahihi kwa wagonjwa.

Pia Soma

Advertisement

Daktari bingwa wa mionzi ya nyuklia kutoka Hospitali ya Ocean Road, Tausi Maftah amesema mashine hizo zinaweza kugundua ugonjwa unaoanza lakini pia kwa wagonjwa walio mahututi iwapo kuna kiungo kimeshakufa ikiwemo Ubongo, moyo na viungo vingine.

“Kwa hospitali ya Ocean Road pekee tunapima wagonjwa kama 30 kwa siku ni mashine zenye uwezo mkubwa.” Amesema Dk Maftah.

Chanzo: mwananchi.co.tz