Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo wa kuratibu dawa kiteknolojia waiva

94fa5c1d3bc7f40640593ad3e12690f7.png Mfumo wa kuratibu dawa kiteknolojia waiva

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya mfumo wa kiteknolojia utakaotambua dawa na vifaa tiba vinavyotoka kwa lengo la kutatua kero katika utoaji wa huduma afya.

Naibu wa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) David Silinde amesema hayo bungeni Dodoma na kuongeza kuwa mfumo huo utakuwa suluhisho la tatizo hilo.

Silinde ametoa maelezo hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Sumve, Kasalali Mageni aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuweka utaratibu utakaosadia kutatua tatizo la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati.

Silinde amesema serikali imekuwa ikipeleka dawa lakini haziwafikii walengwa kama inavyokusudiwa kutokana na baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu ama kwa kuuza dawa hizo au wengine kutozitumia hadi muda wa matumizi unakwisha.

Katika kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi nchini Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga Shilingi bilioni 263.8 kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Chanzo: www.habarileo.co.tz