Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo mmoja sekta ya afya utasaidia utoaji huduma

Dkt Mollel Awasimamisha Kazi Mganga Mkuu, Mganga Mfawidhi.jpeg Mfumo mmoja sekta ya afya utasaidia utoaji huduma

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema wanakwenda kuangalia namna wanayoweza kutengeneza mfumo mmoja wa kidigitali wa afya ambao utaunganisha kuanzia hospitali ya Taifa hadi ngazi ya zahanati.

Mfumo huo ambao unatajwa kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za afya, pia utaunganisha taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za afya ikiwemo taasisi za kifedha na mfuko wa bima wa taifa.

Dk Mollel amesema hayo jana Jumatano, Agosti 2, 2023, jijini Dar es Salaam wakati akizindua Chama cha Wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika sekta ya afya (TAHIA).

Amesema kuwapo kwa mfumo huo utasaidia kufanya ufuatiliaji wa vitu vinavyohusu afya na hata kupata taarifa sahihi ili uamuzi uweze kufanyika ambapo utapunguza gharama na usumbufu kwa wananchi.

“Kwa mfano, mtu anaweza kwenda hospitali ya mkoa akapiga CT-Scan baada ya siku chache akaenda hospitali nyingine ya Kanda au Taifa akarudia tena kupiga bila sababu ya kitiba ni upotevu wa muda na feda,” amesema

Naye Rais wa TAHIA, Sosthenes Bughume amesema mfumo huo ukifanikiwa utakuwa unahusisha asasi nyeti zinazoshiriki katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii. Sehemu ya malengo makuu ya TAHIA ni kupitia maendeleo ya utekelezaji wa mkakati wa afya wa kidijitali wa Tanzania 2019-2024 na mipango ya uwekezaji kwenye afya ya kidijitali na mabadiliko ya kidijitali katika utoaji wa Huduma ya Afya ya Msingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live