Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mewata yasema bora kinga kuliko tiba

10318 Mewata+pic TZW

Fri, 29 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uwekezaji wa fedha katika kinga ya maradhi yasiyoambukiza umetajwa kuwa na faida kuliko gharama za kuyatibu.

Hayo yamesemwa Juni 28, 2018 na mwenyekiti wa chama cha madaktari wanawake (Mewata), Faraja Chiwanga wakati wa mjadala wa Jukwaa la Fikra kuhusu maradhi yasiyoambukiza ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Dk Faraja amesema kwa kulitambua hilo, Mewata inatoa elimu ya namna ya kubadili mfumo wa maisha jambo linalosaidia kupunguza maradhi hayo.

"Uchunguzi wa maradhi hayo ni njia itakayosaidia kutambua ugonjwa katika hatua za awali na kurahisisha matibabu yake," amesema Dk Faraja.

Chanzo: mwananchi.co.tz