Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge atilia shaka MSD

WhatsApp Image 2021 09 04 At 1.52.39 AM.jpeg Mbunge atilia shaka MSD

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akichangia jana bungeni kwenye Muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne wa mwaka 2021, Mbunge huyo amesema MSD imeshindwa kuonesha ufanisi kwenye usambazaji dawa hivyo hadhani kama itaweza kwenye uzalishaji.

"Bohari inatakiwa iwe na usambazaji na kuzalisha,  nilisema wakati wa Bunge la bajeti MSD imeshindwa mara nyingi katika suala zima la usambazaji wa dawa lakini Leo hii inahitaji tena ijiongezee jukumu la kuzalisha, Mimi kwa mawazo yangu sioni kama MSD ina uwezo wa kuzalisha,"amesema.

Pia amesema wakati Bunge linajadili Muswada wa kuwezesha MSD kuzalisha vifaa tiba na dawa lakini ana taarifa kuwa imeanza uzalishaji kabla ya sheria kupitishwa.

Spika wa Bunge Job Ndugai, amemwambia Mbunge huyo kuwa MSD ikianza kuzalisha baadhi ya Dawa hapa nchini itapunguzia serikali mzigo wa kuagiza dawa nje ya nchi.

Chanzo: ippmedia.com