Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka tohara iwe lazima kwa wanaume wote

Hospitali Ya Temeke Yamfanyia Upasuaji Mtu Mwenye Jinsia Mbili.jpeg Mbunge ataka tohara iwe lazima kwa wanaume wote

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Mukurweini nchini Kenya, John Kaguchia anatarajia kuwasilisha muswada bungeni unaotaka tohara kwa wanaume wote kuwa lazima.

Mbunge huyo amedai muswada huo utakapopita na kuwa sheria utasaidia kupunguza magonjwa ya zinaa nchini humo.

Aidha, Kaguchia amesema muswada unalenga kupiga marufuku tohara za kitamaduni ambazo hufanywa na mangariba na hivyo zoezi hilo litakuwa likifanyika hospitalini.

“Kuruhusu muswada wa tohara kufanyiwa hospitali chini ya uangalizi wa wataalamu wa matibabu kunalenga kuimarisha afya njema kwa watoto kuanzia wanapozaliwa hadi pale watakapofikisha miaka 18,” amenukuliwa na tovuti ya Taifa Leo ya nchini humo.

Kaguchia ameongeza kuwa tohara itafanyika hospitalini huku mchakato mwingine wa kitamaduni kuendelea baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live